Leviticus 1:7-9

7 aWana wa Haruni kuhani wataweka moto juu ya madhabahu na kupanga kuni juu ya huo moto. 8 bKisha wana wa Haruni kuhani watapanga vile vipande vya nyama, pamoja na kichwa na mafuta ya huyo mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. 9 cAtaziosha sehemu za ndani na miguu yake kwa maji, naye kuhani atavichoma vyote juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, yenye harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

Copyright information for SwhKC